TununuePamoja ni nini?

TununuePamoja ni moja kati ya huduma zitolewazo na kampuni ya Bero Investment & General Supply kupitia project yetu ya ununuzi wa bidhaa mtandaoni (BeroGenge). TununuePamoja ni mfumo mpya na kupitia Mfumo huu tunakuwezesha kuagiza bidhaa kutoka China kwa kushirikiana na wengine ili kuweza kufikia kiwango cha Chini (MOQ) kinachopangwa na viwanda au wachuuzi wakubwa na kujipatia bidhaa kwa bei nafuu.

Tumelenga nini hasa?

Ni ukweli usiopingika kwamba upatikanaji wa bidhaa kutoka China ni nafuu katika suala la bei na ni ndoto ya wafanyabiashara wengi kuweza kupata bidhaa moja kwa moja kutoka China. Lakini tatizo kubwa linalowakwamisha wengi ni uwezo wa kufikia kiwango cha chini cha kununua bidhaa yaani MOQ, kwani mara nyingi itakuhitaji ununue kiwango kikubwa ndipo upate kwa bei nafuu. Kutokana na uwezo wa mtaji au mipangilio mingine ya kibiashara suala hili ya MOQ linakwamisha wengi kununua bidhaa kutoka China.

Tunafanya nini hasa?

TununuePamoja.com kwa umakini na umahiri tunahakikisha upatikanaji wa bidhaa zilizo bora, tunapokea oda zako, tunahakikisha pesa zako zipo salama na tunafanya malipo ya oda zako sehemu husika, tunakusafirishia mzigo hadi kwenye stoo zetu na pia tunahakikisha kila mmoja anapata mzigo wake kulingana na idadi aliyoagiza. Mfumo huu ni rahisi kutumia na ni rafiki kwa mtumiaji.

Tunapatikana wapi?

Ofisi na stoo yetu ipo karibu na kituo cha daladala Bamaga barabara ya Sinza Dar es Salaam, Wasiliana nasi kwa+255745 260 019 (Call & SMS), +86 17858995075 (Whatsapp)

Tunasafirishaje mizigo?

Kwa kawaida mizigo tunasafirisha kwa njia zote yaani njia ya ndege na njia ya meli na tunajitahidi katika kuchagua kampuni ambazo zinasafirisha mizigo kwa uharaka na uhakika.

Mizigo inachukua siku ngapi kufika stoo yetu?

Inachukua mwezi na nusu hadi miezi miwili kwa usafiri wa maji. Na inachukua wiki moja hadi mbili kwa usafiri wa ndege.

Vipi kuhusu watu wa mikoani?

Tayari BeroGenge tumeanza kujitanua kuwafikia watu wa mikoa mingine, na baadhi ya mikoa tayari tuna mawakala na tunaendelea kutafuta mawakala zaidi kufikia mikoa yote ya Tanzania. Utaratibu wa sasa, baada ya mizigo kufika stoo yetu utatumiwa kama upo mkoa mwingine.

Tunajivunia zaidi ya wateja 10000 walioridhika na huduma zetu
Ubora wa bidhaa
Usafiri wa haraka
Huduma nzuri kwa wateja